G.S. Muse
6 min readApr 27, 2024

Mfano wa Shimo The Parable of The Pit — Swahili Edition

Siku moja mtu mmoja alikua akitembea ndani ya msitu punde tu aliposikia sauti ikiitana
“kuna mtu hapo anisaidie”
Adinasi huyu anaiacha njia yake na kuingia kilindini mwa msitu
“Nakusikia,uko wapi?”anauliza.
“Ndani hapa!”Sauti inasikika.
Mja huyu hamuoni yeyote lakini ana kata shauri kuelekea kunakotokea sauti ile hadi karibu na ukingo wa shimo lililo wazi lisiloweza kuonekana vizuri kutokana taswira mbovu na uchavu kwenye msitu.
“Je,unaweza kunisaidia?”Mtu aliyeketi ndani ya shimo alimuuliza. “Nimekwama hapa kwa muda mrefu na hakuna aliyejitokeza kupita hapa”aliendelea kusema. “ulitumbukia vipi?”aliulizwa. “Nilikua nikitembea punde nilipotumbukia ghafla kwa shimo ambalo sikuanimeliona kwa wakati”alijieleza. “je wahitaji nikutafutie msaada?” mtu wa kwanza aliuliza. “Nimekua hapa kwa muda sasa hili shimo limekua tatizo kubwa kwangu,je, waweza kutenga muda tuzungumze kwanza kabla haujaenda kunitafutia msaada?”alizungumza kwa unyenyekevu. mtu yule alikubaliana na ombi lake.
Wawili waliketi na kuzungumza kwa muda huku akimwelezea simanzi na woga uliosababishwa na dhiki ile kutazama jua lililokua likitua angani mtu yule akawaza na kusema “natumae nina Kamba nzuri na nzito kwenye mfuko wangu ulio na uwezo wa kudhibiti uzito wa mtu” akaufunga kwenye mti na kurusha sehemu nyingine ndani huku amebakisha sehemu kiasi ya kushikilia.Mtu yule hakudhubutu kusimama, alipoitazama Kamba ile kwa wasiwasi, akamweleza yule aliyekua shimoni “sasa unaweza jivuta huku nje nimelifunga Kamba hili kwenye shina la mti ambao utaweza kudhibiti uzito wako salama salimini”.Siko tayari alimjibu.
“Je twaweza kuzungumza kiasi kabla sijajaribu kujivuta huko nje?” Mtu wa kwanza akakubaliana naye wakapiga gumzo kwa muda jua likizidi kutua angani. Hatimaye mtu aliyekua nje ya shimo alimsihi “sasa waweza toka kwa sabubu jua linazidi kutua na giza litatanda wakati wowote”. “Sasa Naogopa naweza kosa uwezo wa kutumia Kamba hii, je, waweza kua na kitu kingine kando na Kamba hii?”.Mtu yule akakumbuka kibanda kilichokua kimetengwa kwa muda na kilikua mbali kiasi alienda na kulipata ngazi nzee iliyokua na vumbi ingawa ilikua bado kwenye hali nzuri yenye nguvu na uwezo wa kudhibiti uzito wa mtu. Alirejea na kuiteremsha kwenye shimo, mtu yule alipoiona hakudhubutu kusimama ila aliangalia chini badala yake akaitazama sakafu chafu.
“Nini mbaya?” aliulizwa baada ya muda mrefu wa kimya. “Umepata jeraha? kwa nini hutoki nje ya shimo?”. “kwani hunionei huruma? aliyekua kwenye shimo alinungunika. Mtu wa kwanza alistaajabishwa na kuuliza “je, nimesema jambo lolote lililokuudhi?”. “Wewe unanipa ngazi na kutarajia tu niikwe huna hata huruma? huoni nimekwama humu?”. Mtu wa kwanza akawaza kwa muda na kudadisi kwamba mtu yule alikua anapitia dhiki pamoja na kuwa katika hali ya upungufu wa kimawazo akaamua kumuuliza kile angelipenda afanye, mtu yule shimoni akamwabia wawe na mdahalo kidogo kisha baadae atatoa uamuzi wa kile watakachofanya baadae.Shingo upande alikubali na wakatagusana kiasi kwamba jua likawa limezama nyuma ya milima.
“Singelipenda nikukwaze,” Aliyekua nje alisema, sasa unaweza jaribu kutumia Kamba au ngazi giza linaenda kutanda na unaweza kujipata kwenye shimo lingine iwapo hutajinusuru”. “Ni jinsi gani unanidunisha? ukiwa hapo juu unapaswa kuhurumia hisia zangu,”Alifoka kule shimoni. “Najua ni vigumu lakini ukijikaza na kujizatiti waweza kujitoa kwenye shimo kisha hutahisi kusononeka..”
“Kwani unadhani Kamba na ngazi zinaweza kutatua shida zangu zote?” “Haziwezi kutatua shida zako zote ila ilioko sasa ili usiwe katika simanzi ya kuwa katika shimo..?” “kwa hivyo unadhani ni kupenda kwangu kutumbukia katika shimo hili? lakini hujawai patikana ndani ya shimo,ni kwa msingi upi unanihukumu hivi?” “Huenda jua lilikua limezama nusu.” Mtu wa kwanza aliwaza kwa muda huku akijaribu kutazama hali kulingana na mtazamo wa mtu yule atafakari kile angekitenda.. “je, wataka kukwama kwenye shimo?”Mtu wa kwanza alimuuliza huku amechanganikiwa.Mtu wa pili akajibu “inama kisha uushike mkono wangu alafu univute nje.”
“Siwezi fanya hivyo” mtu wa kwanza alijibu, “kwa sababu twaweza kujikuta wote tumenaswa ndani ya shimo hili na pia naweza pata jeraha ambalo laweza kunizuia kujinusuru.Hata hivyo sina nguvu za kutosha ili kudhibita uwezo wa mwanaume mwengine.”aliongezea. “Nadhani niliona koleo, pengine unaweza kuitumia kutengeneza ngazi itakayo kuwezesha kujinasua nje, je,ungependa nikulete?” Mtu wa pili akajibu kwa sauti ya chini na dhaifu “….ndio..” Wakati huo jua lilikua sasa halionekani vizuri juu ya milima.
Punde tu mtu yule aliporejea na koleo giza lilikua tayari limetanda ilimbidi atembee kwa utaratibu na uangalifu ili pia naye asitumbukie shimoni… “uko wapi?”aliuliza kwa sauti… “niko hapa” yule mwengine alimjibu.Akafika ukingo wa shimo ile huku mwezi ukiwa umeanza kungaa nyuma ya mawingu… “niko na koleo ila giza lanitatiza kuona uliko, naenda kulitupa katika ukingo huu ili isikudhuru.” Yule mtu shimoni hakusema lolote.Mtu wa kwanza alitumbukiza koleo ndani ya shimo akalisikia likianguka sakafuni,mtu yule shimoni hakusikika akifanya lolote wala kusonga.
Je, umeona koleo? waweza kutengeneza njia yako nje?” Aliulizwa.Kulikua na ukimwa kwa muda. “je, uko sawa?” Mtu nje ya shimo sasa aliuliza. “Wacha kunilazimisha kufanya mambo kulingana na mtazamo wako” Mtu ndani ya shimo alijibu. “nimejaribu kila kitu na imekua ngumu mimi kutoka kwenye shimo hili,umekuja hapa na Kamba,ngazi na koleo ukidhani wewe ni bora kuliko mie, kuonekana kwamba mimi ninafanya vibaya” mtu wa nje akapumua pumzi nzito na kusema “najua hali yako ni ngumu kwa kiwango tofautitofauti lakini nimekupa Kamba,ngazi na koleo ujaribu kutoka nje..utaenda kusimama uchukue moja wapo ya vifaa hivyo ujaribu kutumia kupata nafasi ya kujiokoa mwenyewe?”
“Vipi unanihukumu? wewe huko bora kuniliko,ingelikua ni wewe umenaswa humu ndani ungehisi ninavyo hisi na ungeitaji mtu akuonee huruma, ungetaka wakuhurumie.” Mtu yule nje hakusema lolote kwanza alitazama miti mieusi na kutumania nuru kiasi kutoka kwa mwezi, alipogundua kuwa sio mengi angemtendea mtu yule na ilhali alikua kwenye hatari ya kusafiri usiku huku akijaribu kumnusuru mtu yule “sasa mimi naondoka, uko na Kamba yako,ngazi yako na koleo yako, ukikataa kuvitumia utakuwa umenaswa ndani ya shimo hilo au pengine kuna mtu atakuja akuvute nje, nimekupaa vifaa na wewe lazima aghalabu ujikaze kuvitumia ili kujipatia uhuru wake.”
Mtu wa kwanza akaanza mwendo kuondoka punde tu kilio kingine kikitokea shimoni “…ni…sa..i….die………” huku sauti ikipotea,mtu huyo alitembea hadi akateleza karibu kuanguka kwenye shimo lakini akabahatika kujinasua nje na kuangukia mgongo hadi chini akilia kwa uchungu, anasimama huku akijikunguta mavumbi na matawi libasini.
“…kuna mtu hapo..?”sauti iliitana. Aligundua kuwa kulikuwa na shimo mbele yake na akashangaa iwapo amekua akizunguka ndani ya shimo lakini akagundua kuwa sauti hiyo haikuwa kama ile ya kwanza hiyo ilikuwa nzito kama ya mtu ambaye amekula chumvi nyingi “..niko hapa!” mtu wa kwanza alijibu “..oooh ahsante mungu,” sauti iliyoridhika ilisikika” “..nilianguka katika shimo hili na nimeshindwa kujitoa mwenyewe…” “laiti ningekua na uwezo wa kukusaidia,” mtu wa kwanza alisema. “lakini niliwacha Kamba yangu mbali kidogo kwa kuni na na hofia siwezi kuipata tena kwa sababu ya giza..”
“Nina kamba ..sauti nzito ilisikika ikitoa suluhu, “nikikurushia unaweza kuufunga kwenye mti ili niweze kujinasua?”....mtu wa kwanza bado alikuwa katika hali tata iwapo anejaribu kumsaidia mtu mwengine haswa wakati huo wa usiku na alikua tayari anataabika kupata njia ya kuridi alikotoka.Lakini alikubali ..alichukua Kamba na kuifunga kwenye shina la mti..haikuwa dhabiti kama mti ule mwingine kwenye shimo la kwanza lakini ingesaidia..akapaza sauti “..nimeifunga!..waweza kukwea sasa!..kamba ikajinyosha mzee alipokua akijinasua nje.. “ahsante!” alisema.
“Nimekwama ndani ya shimo hilo siku nzima nikijaribu kutafuta mbinu za kujitoa nje ningelikaa hapo kwa muda singelijua cha kufanya .” Mtu wa kwanza alipata afueni kwa sababu juhudi zake za kuokoa huyo mtu wa pili hazikuambulia patupu.. “Iwapo kuna jambo lolote dogo ambalo nawezakufanyia kama njia ya shukurani usisite kuniomba..” mtu wa kwanza aliitikia kwa ishara ya kutingiza kichwa kwa vile huyu wa pili aliweza kumwona kwenye giza.
“Jambo la kusikitisha sote twaweza kuwakatika hali ngumu,waweza kuwa huru kutokana na shimo lakini tatizo ni kwamba sote tumepatikana katika msitu huu.
“Sina uhakika jinsi ya kujikwatua kutoka kwalo kutokana na giza na sina mwanga.”Alisema.
“Nina mwanga” mtu mwengine akasema.
Alipekuapekua kutoka kwenye mfuko wake na kutoa kitu.Ilikua ni kipande cha mbao kilizungukwa na majani ya mabwawa na aina nne kadha ya uyoga unaongaa,kila moja na rangi ya aina yake.Kipande hicho kilitoa nuru ya kutosha ndani ya msitu uliomzunguka pia sehemu za mwili wa mtu.
Alikua na umri kumliko yule mtu wa kwanza,mwenye nguvu na mjasiri usoni mwake na mwenye macho makavu.
Wawili hao walitembea kwenye msitu hadi wadi waliposikia sauti nyingine ikiita kwa sauti kutoka kwenye shimo pakiwa na hakuna wa kumpa mkono wa usaidizi.
Wlitumia Kamba ile ambayo yule mzee aliitumia kujinasua nje ya shimo alilo kuwa amekwama ndani akaifunga kwenye mti na yule mtu akaitumia kujiweka huru.
Mtu wa tatu akawashukuru wasafiri wale wawili na kwa pamoja wakaendelea na safari na kuwaokoa wengine wengi walikutana nao katika safari yao ya kuelekea katika mji mahali ambapo mtu wa kwanza aliishi.Wengine walikuwa katika hali ya kusononesha na kuhuzunisha kabla watu wale kuwanasua kutoka kwenye shimo lakini kila mmoja wao alitoa shukrani zake za kuwekwa huru.
Punde tu walipofika katika mji marafiki wale kila mmoja alienda zake kuelekea nyumbani kwake ama ukingoni.
Hatimaye watu wale wawili walisimama pamoja nje ya nyumba ya mtu wa kwanza.Mwenye umri akamwambia “Nashukuru tena kwa kuyaokoa maisha yangu wengi wao hawangelitoboa bila wewe.Umesaidia watu wengi sana leo.Wengi wao wasingeliweza bila wewe.”
Mtu wa kwanza hakuonyesha tabasamu katika uso wake hata,lakini akadadisi kuwa angalishinda na yule mtu ambaye hangeweza kujiokoa pengine angenaswa kwenye msitu ama pia naye angetumbukia kwenye moja ya mashimo yale usiku ule.

Pixabay Image Credit Here
G.S. Muse

G.S. Muse, also known as GreenSlugg on YouTube or simply as “Greg” is a lab technician, youtuber, author, and blogger. His work can be found at GSMuse.com